Tuesday, June 23, 2009

BIFU LA UFISADI MENGI VS. ROSTAM NANI ZAIDI?

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa, hivi sasa kumeibuka makundi makubwa mawili ndani ya jamii, moja likiwa upande wa Mengi na lingine likiunga mkono kambi ya Rostam.Mbali na serikali kusitisha malumbano hayo, kupitia Naibu Waziri wa Wizara ya Habari na Michezo, Mh. Joel Nkaya Bendera, bado msuguano unaendelea chini ya kapeti, huku baadhi ya watu wakionesha moja kwa moja upande wanaouunga mkono.

Ilidaiwa kuwa, serikali iliufunga mjadala huo rasmi lakini makundi hayo yamekuwa yakiendeleza libeneke hilo mitaani jambo linalojenga hofu ya baadaye. Wakizungumza na Amani kwa nyakati tofauti, wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa hapa nchini walitonya kuwa, malumbano hayo ni dalili ndogo ukilinganisha na hali halisi ambapo walibainisha kuwa itakuwa mbaya zaidi huko mbele ya safari.“Bado moshi juu ya tuhuma za ufisadi unafukuta, moto kamili ni huko tuendako kwa sababu chuki inazidi kuongezeka kila kukicha miongoni mwa kundi linalomuunga mkono Mengi na lile la Rostam, ukweli hali itakuwa mbaya zaidi hapo baadaye kama mjadala wa wazi usipofanyika,” alisema mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamesema ni vyema kama vigogo hao ambao walilumbana kwa ishu ya ufisadi wangewekwa chini na kufanyika kwa mjadala wa wazi ambao ungetoa suluhu ya kudumu kuliko serikali kudhani mambo yameisha wakati siyo

No comments: