MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ameumbuliwa bungeni, kuwa amepewa wadhifa huo kinyume cha taratibu.
Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi, huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania.
Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.
“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.
Mporogomyi aliliambia Bunge kuwa sifa za mkurugenzi huyo ni kwamba ni mshauri wa mambo ya ununuzi na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa anafanya shughuli zake visiwani Zanzibar.
Hata hivyo, Mrema mwenyewe alijitetea kuwa ana shahada ya kwanza ya ukandarasi uchumi (Construction Economics) na shahada ya pili ya Menejimenti ya miradi (Project Management) aliyoipata mwaka 1987. Hata hivyo, hakutaja vyuo alikopata shahada hizo.
Aliwataja wahandisi ambao walipendekezwa na jopo la usaili kuwa ni Boniface Nyiti, Venance Ndyamkama na mwingine aliyemtaja kwa jina la moja la Chacha. “Hawa ndiyo ambao walipendekezwa na ni wahandisi wa siku nyingi pale Tanroads; lakini huyu mkurugenzi alikotolewa na kuwekwa pale haijulikani.”
Mrema alichukua wadhifa wa mkurugenzi aliyekuwa anatokea Ghana ambaye alimaliza muda wake mwaka 2006. Mporogomyi alisema mkurugenzi wa sasa aliingizwa kwa misingi ya ufisadi.
Mbunge huyo aliongeza kuwa mara tu baada ya kupata wadhifa huo, alianza kuwanyanyasa wahandisi hao wenye sifa na akawahamishia wizarani ambako pia walirudishwa na wizara Tanroads. “Wizara ilisema hawa ni mawakala wa ujenzi wa barabara wakawarudisha.”
Alisema Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu wakati inawarejesha kwa Tanroads, ilishauri wapewe mikoa ya kuongoza, lakini kuwa tayari nafasi hizo zilishajazwa na watu wengine Mrema hakuweza kutekeleza agizo hilo.
Alisema alibaki nao makao makuu na wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi za kufanya. Alisema kuwa mkurugenzi huyo baada ya kuona wahandisi hao ni tishio katika ajira yake, sasa ameingiza utaratibu mpya wa ajira za mikataba.
Mporogomyi alisema mpango huo mpya unafanywa na mkurugenzi huyo kwa nia ya kuwaengua wafanyakazi wote ambao anaona kama ni tishio kwake, hasa wale wahandisi wenye sifa za kushika wadhifa wake huo.
“Kibaya zaidi pamoja na kuingia kwa mlango wa nyuma, lakini ananyanyasa wafanyakazi,” alisema mbunge huyo huku akimtaka Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu amweleze namna mkurugenzi huyo alivyoingizwa kwenye nafasi hiyo nyeti na ikiwezekana aondolewe haraka.
Lakini pia alisema mkurugenzi huyo analipwa fedha nyingi kama vile ni mtaalamu ambaye ameajriwa kutoka nje ya nchi.
Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).
Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.
Mporogomyi alisema pamoja na fedha nyingi anazolipwa mkurugenzi huyo; lakini bado anajihusisha na vitendo vya ufisadi zinavyosababisha wakati mwingine awanyanyase na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanatenda haki.
Mbunge huyo alitoa mfano kuwa kuna mfanyakazi aliyemtaja kwa jina moja la Mabuye ambaye alikuwa anafanya kazi katika mizani ya Kibaha. Alisema siku moja mfanyakazi huyo alikamata malori ambayo yalikuwa yamezidisha uzito wa bidhaa walizobeba.
Alisema aliyazuia na kuwataka walipe faini ya Sh milioni 18, lakini matajiri wa yale malori walipoambiwa kukamatwa kwa magari yao walimpigia simu na yeye akaamuru Mabuye afukuzwe kazi.
Mporogomyi alisema Mrema alimpigia simu meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani ili amfukuze na aliposita alimtishia kwa simu kuwa afanye hivyo haraka, kwani hataki kumwona huyo mfanyakazi akiendelea na kazi.
“Kama siyo ufisadi hiki nini, yaani mfanyakazi ambaye anafanya kazi kwa misingi ya sheria unamfukuza kazi, sababu ni nini hapa? Alihoji mbunge huyo na kusisitiza kutaka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri wa Miundombinu.
Tuesday, August 11, 2009
MZUNGU AFANYIWA UFISADI TANZANIA
Subject: FW: RE: MY NIGHTMARE IN TANZANIA
Date: Tue, 4 Aug 2009 15:04:53 -0400
From: Ray Bergen
To: Lisana Koliskowski
Hello Lisa
I am glad to be back in America after such a disastrous trip to Tanzania. The most important thing was getting back home safely and seeing my family. The only thing I can assure you is that, I will never set my foot in that country, and will advice anybody planning to visit Tanzania to refrain from doing so. The nightmare started at the airport, when my luggage checked in from Amsterdam disappeared mysteriously in Dar es Salaam. And my inquiry with the airport authorities was forwarded to the police. At the police station (Central) I was told that I could not get help unless I bribe them $500, because they needed the money for fuel and other necessary needs to investigate the theft. Supposedly the police officer did not open the case and turned me to be the criminal, constantly coming to my Hotel room, asking me for money. In short all my four year work was lost with the laptop at the Airport.
Came clearing the vehicle we were supposed to use in the research, from the agents to the customs authorities, the vehicle exceeded the actual cost. I would have paid $38,000 for a $16,000 vehicle. I could not bear being in such a corrupt country and decided to terminate my research, and left the vehicle uncleared after one month of struggle with the customs, who needed money after money and bogus letters. Supposedly these exuberant fees were not supposed to be there in the first place, because all registered NGO’s are supposed to be exempted from paying these taxes and fees, but then the deal had been cooked to rip Muzungu off. Being a Muzungu is being a cash cow in Tanzania. They don’t even fucken know that we are trying to help them. I pity the African continent and her people, I am glad they did not confuse me with Albino
Please advise any potential traveler to Tanzania to look for alternative country to visit, and if possible pass the message to the State Department as a warning to other Americans intending to visit this poor and corrupt country. I visited Botswana with my family in 2006. I tell you, could not be more satisfied with their politeness and straightforwardness, the same was in Mozambique where we received utmost hospitality.
Please, be careful and only travel to Tanzania when there is need and not to visit and do not carry any valuable. As soon as you arrive, register with the American Embassy
Sincerely,
Ray Bergen

Monday, August 3, 2009
UFISADI NDANI YA UMASIDA.........!!
UMASIDA ni umoja wa matibabu secta isiyo rasmi DSM , ilianza mwaka 1994 na kuwa registered 1997 society namba 8907,
Umasida iliundwa na board of director, director pamoja na department 4 ambazo ni social mobilization, advocacy, health services, finance and administration
Umasida its offer
• Maternal child health care services
• Treatment for regular diseases like malaria, diarrhoea
• Provided VCT na STI MGT
• Surgical needs, ENT and ophthalmic provide at gvt unit
Kwa mafanikio makubwa yaliyotokea mwanzoni iligundulika kuwa ni secta iliopata mafanikio makubwa kwa miaka ya mwanzoni ,
Kutokana na wrong price ya umasida ilipelekea Tanzania iwe na fund short fall 80% 2006
UMASIDA inaweza kufananishwa na taasis nyingi zilizoleta mafanikio nchi nyingi kama SEWA AND TATA /AIG in india, la equided in Colombia, serviperv in peru IFP/ SSE in bukinafaso , ila si Tanzania
Kwa kuona umuhimu wa maendeleo ya nchi yetu kunasecta nyingi ambazo hivi sasa zinaleta mafanikio kama MKUKUTA, MKUZA, AMREF. Ingawaje TACAID iliweza kuwa benet sana na UMASIDA haikuweza kutowa matunda amabayo wananchi wa dare s salaam na Tanzania mzima walikuwa wanayasubili, mfano mwaka 2005 gazeti moja la IPP liliweza kutowa habari ya Umasida kusimamisha wafanyakazi wa wili kwa financia fraud,hata ivyo haikuzaaa matunda.
Ingawaje mh: Rahisi wetu anakuwa omba omba ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ya kisasa ila bado wafanyakazi wake kama vile UMASIDA wanamtupa mkono.
Unaweza ukasema ufisadi upo Richmond , Tanesco , Tics kumbe kuna jungu la ufisadi ambao serikali inalinyamazia kimya na wanajifanya wanachunguza kwa kipindi kirefu zaidi .
Unaweza sasa ukafananisha na UMASIDA ivi sasa inakaribia mwaka na nusu au miwili tangia umasida iishe kabisa kwa manufaa ya wachache ambao ni top line staff ambao waliweza tumia pesa za taasisi kwa manufaa yao binafsi na kujiimalisha kimaisha, japo tume iliundwa na ikatowa ikaanza kazi kwa kumuoji mkurugenzi wa taasisi hiyo ila imechukuwa muda mrefu bila yakutowa majibu.
Kama ni taasisi ilioyokuwa itowe uduma kwa wananchi imekuwa kinyume na mategemeo na ikatowa nuduma kwa wachahe ambao nchi, wizara iliwaamini nabado inawaangalia macho je wakienda taasisi nyingine maendeleo yatakuwa wapi hapo.
Kwa upelelezi tulioufanya kipindi kichache sasa ilileta habari kuwa serikali halijalinyamazia kimya bado lipo kwenye mchakato wa uchunguzi ila si muda mrefu wahusika watafikishwa mahakamani wakiwemo head of departments, mkurugenzi na wahasibu ambao walitumia pesa za taasisi kununua magari ya galama kujenga majumba ya galama na kufanya uwekezaji tofauti uku walengwa wanakufa kwa kukosa matibabu na uduma husika.
Hata hivyo kama uchunguzi wa kesi unachukuwa muda mrefu je hizo pesa ambazo hao watu wamechukuwa je zitakuwepo, je hao watu watakuwa hawajafanya financial fraud sehemu nyingine tofauti, je uchumi na maendeleo ya nchi yatakuwepo.
Kama hatutashirikiana kufichuwa ufisadi kamwe hautaweza kuisha , kuna taasisi nyingi sana ambazo zimekufa kama umasida na serikali inaangalia macho,
Kama walengwa hawatafaidika na mambo ambayo walistahiri CCM mnajipalilia motto mgumu sana , sio kama watu hawaoni nini kinaendelea tuansubili utekelezaji wa serikali yetu tulio iamini na kuitegemea kwenye maendeleo na kukomesha ufisadi

FISADI MKUU TANESCO DR IDRIS RASHID
MBUNGE wa Sumve (CCM), Richard Ndasa ameibua ufisadi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kulieleza Bunge kuwa shirika hilo liko katika harakati ya kuiuza kwa Sh60 milioni nyumba namba 13 iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Toure/ Chaza line baada ya kuikarabati kwa Sh600 milioni.
Sambamba na ufisadi huo, pia Shirika hilo linatuhumiwa kutumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba sita za wakurugenzi kinyume na taratibu.
Ndasa alitoa tuhuma hizo nzito bungeni jana alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa Jumamosi iliyopita na waziri wake, William Ngeleja.
Ndasa alisema fedha hizo ambazo ni sehemu ya mkopo wa Sh280 bilioni iliyochukuliwa benki kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo ya Tanesco, imetumika bila idhini ya bodi ya wakurugenzi.
"Tanesco kuna matatizo makubwa yanayotokana na usimamizi mbovu na matumizi mabaya ya fedha. Shirika halina vipaumbele, linatumia vibaya fedha za umma," alisema Ndasa na kuongeza:"Mwaka 2007 shirika hilo lilikopa Sh280 bilioni kutoka benki mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini badala ya kutekeleza vipaumbele, limeamua kukarabati nyumba za wakubwa kwa zaidi ya Sh1.4 bilioni".
Mbunge huyo alitaja nyumba zingine zilizofanyiwa ukarabati huo na gharama zake kwenye mabano kuwa ni namba 89 iliyoko Barabara ya Guinea (Sh250,463,140), namba 65 iliyoko Barabara ya Lisbon (Sh 190,407,430) na namba 159 iliyoko mtaa wa Mawenzi iliyokarabatiwa kwa Sh130 milioni.
Nyingine ni nyumba namba 93 Barabara ya Guinea (Sh 88,515,820), namba 315, Mtaa wa Toure Drive ( Sh79 milioni) na namba 98 iliyoko katika Barabara ya Uganda iliyokarabatiwa kwa zaidi ya Sh730 milioni.
"Bodi ya wakurugenzi haikuidhinisha matumizi ya fedha hizo," alisema Ndasa ambaye pia alifafanua kuwa mkopo wa fedha hizo utatakiwa kurudishwa na wananchi kupitia bili za umeme.
Akizungumza nje ya Ukumbi wa Bunge, Ndasa alifafanua kuwa nyumba namba 13 iliyoko Oysterbay iliyokarabatiwa kwa zaidi ya Sh600 milioni, inakaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Idris Rashid ambaye amebakisha miezi mitatu kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu, ametuhumiwa kujipangia kuinunua kwa Sh 60 milioni.
Kimahesabu nyumba hiyo itakuwa imeuzwa kwa asilimia 10 ya thamani ya kuikarabiti, mbali na thamani yake halisi pamoja na gharama za kiwanja hicho kilichoko eneo la Oysterbay ambayo ni ghali.
Kwa mujibu wa Ndasa, matumizi hayo ya fedha za mkopo unaopaswa kurejeshwa kwa kiasi cha Sh4 bilioni kila mwaka kuanzia mwakani, ni mabaya na ndiyo yanayochangia shirika hilo kushindwa kusambaza umeme vijijini.
Kauli ya Ndasa iliungwa mkono na Mbunge wa Busega Raphael Chegeni (CCM), aliyelieleza Bunge kuwa Tanesco inapitia misukosuko ya mfumo wa kiutendaji.
Alisema shirika hilo ambalo Watanzania waliamini uongozi mpya ungewasaidia baada ya kuondolewa kwa kampuni ya Net Group Solutions ya Afrika Kusini, lina matatizo makubwa ya usimamizi wa fedha na vipaumbele.
"Wakati tunaifukuza Net Group Solutions tulijua sasa tumemaliza tatizo, kumbe ovyo. Tumeshuhudia Tanesco ikipitia misukosuko mingi ya kimfumo na utendaji na kuonekana kuwa na tatizo kubwa la usimamizi wa fedha," alisema na kuongeza:"Mimi naomba katika bajeti hii tuangalie tunabadilishaje mfumo huu. Tunahitaji kujua lini Tanesco itamalizia miradi ya umeme vijijini.Tutakuzaje uchumi kama nchi haina umeme?".
Naye Mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongela (CCM) aliwataka wafanyakazi wa Tanesco kuongeza kasi ya utendaji ili shirika likamilishe miradi ya umeme vijijini.
"Wafanyakazi Tanesco acheni uzembe, we are serious (hatutaki mzaha) kwani hata kama hamna fedha; hizo kidogo mlizonazo mnaweza kuzitumia vizuri na kwa uangalifu zikaleta matunda yaliyokusudiwa," alisema Mongela.
Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo nje ya Ukumbi wa Bunge, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Idris Rashid aligoma akisema, "Haya ni masuala ya Bunge atayajibu waziri". Alipoulizwa zaidi kwamba, haoni tuhuma hizo zimeelekezwa kwake moja kwa moja alijibu kwa mkato zaidi, ”Nasema sisemi chochote, hili ni Bunge".
Mwaka juzi uongozi wa Tanesco ulisema unahitaji mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ili angalau kuliweka katika hali nzuri ya kuweza kutoa huduma ya umeme nchini.
Thursday, July 16, 2009
VITA DHIDI YA UFISADI NDIO UNAANZA, TUMENI HABARI NA PICHA
WATANZANIA, TUMECHOKA NA UFISADI, HII BLOGU IMEANZISHWA RASMI KWA AJILI YA KUUPINGA UFISADI. HAKUNA KITAKACHOZUILIWA LINAHUSIAANA NA UFISADI. PICHA ZA NGONO NA HUTUPU HATUTAKI LAKINI ZA UFISADI ZOTE ZINAKARIBISHWA
TUNAOMBA HABARI ZOTE NA PICHA ZINAZOHUSIANA NA UFISADI. MICHUZI ANAOGOPA, HAPA JIRANI SISI TUNAJICHUKULIA SHERIA YA KUWAANDAMA NA NI LAZIMA TUWAKOMESHE. HAPA HAKUNA MAJUNGU NI UKWELI, UFISADI LAZIMA TUUKOMESHE
MAPAPA
ROSTAM
CHENGE
MKAPA
LOWASSA
SUMAYE NA TAKATAKA ZOTE LAZIMA WALIONJE JOTO LA JIWE
TUMA HABARI KUPITIA Jamiiforums@yahoo.com . KADHALIKA UNAWEZA KUTUMA PICHA ZA MAFISADI UNAOWAJUA, WALA RUSHWA, NAKADHALIKA, TAJA WANAKOFANYA KAZI, NYADHIFA ZAO NA KADHALIKA......
TANZANIA DAIMA
JAMIIFORUM DAIMA

Tuesday, June 23, 2009
FISADI KIONGOZI ORIGINAL TANZANIA
Huyu mtu ameimaliza Tanzania, lakini cha kushangaza ni kwamba bado yuko huru
Tumeni maoni na picha kupitia Jamiiforums@yahoo.com Maoni yote, picha zote isipokuwa za Utupu hazitakubalika, ila mengineyo yote yanakaribishwa na yatachapishwa
Tumeni maoni na picha kupitia Jamiiforums@yahoo.com Maoni yote, picha zote isipokuwa za Utupu hazitakubalika, ila mengineyo yote yanakaribishwa na yatachapishwa
BIFU LA UFISADI MENGI VS. ROSTAM NANI ZAIDI?
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa, hivi sasa kumeibuka makundi makubwa mawili ndani ya jamii, moja likiwa upande wa Mengi na lingine likiunga mkono kambi ya Rostam.Mbali na serikali kusitisha malumbano hayo, kupitia Naibu Waziri wa Wizara ya Habari na Michezo, Mh. Joel Nkaya Bendera, bado msuguano unaendelea chini ya kapeti, huku baadhi ya watu wakionesha moja kwa moja upande wanaouunga mkono.
Ilidaiwa kuwa, serikali iliufunga mjadala huo rasmi lakini makundi hayo yamekuwa yakiendeleza libeneke hilo mitaani jambo linalojenga hofu ya baadaye. Wakizungumza na Amani kwa nyakati tofauti, wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa hapa nchini walitonya kuwa, malumbano hayo ni dalili ndogo ukilinganisha na hali halisi ambapo walibainisha kuwa itakuwa mbaya zaidi huko mbele ya safari.“Bado moshi juu ya tuhuma za ufisadi unafukuta, moto kamili ni huko tuendako kwa sababu chuki inazidi kuongezeka kila kukicha miongoni mwa kundi linalomuunga mkono Mengi na lile la Rostam, ukweli hali itakuwa mbaya zaidi hapo baadaye kama mjadala wa wazi usipofanyika,” alisema mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamesema ni vyema kama vigogo hao ambao walilumbana kwa ishu ya ufisadi wangewekwa chini na kufanyika kwa mjadala wa wazi ambao ungetoa suluhu ya kudumu kuliko serikali kudhani mambo yameisha wakati siyo

Subscribe to:
Posts (Atom)